Saturday, 26 March 2016

Iran yakana kuidukua Marekani

Iran yakana kuidukua Marekani

Iran imekanusha kuwa iliidhinisha mashambulio ya mitandao dhidi ya Marekani, baada ya mahakama mjini New York, kuwashtaki raia saba wa Iran, kwa kufanya udukuzi huo.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Iran, (Hossein Jaberi Ansari), alieleza kuwa Marekani haina haki ya kushtaki raia wa nchi nyengine, bila ya kutoa nyaraka za ushahidi.
Alisema Marekani yenyewe ina historia ya kufanya udukuzi dhidi ya Iran.
Wadukuzi hao wameshtakiwa kwa mashambulio kwenye mitandao ya mabenki kadha ya Marekani, na bwawa la New York, baina ya mwaka 2011 na 2013.
Washtakiwa wote wanaishi Iran, na waandishi wa habari wanasema, haikuelekea kuwa watapelekwa Marekani kukabiliwa na mashtaka

No comments:

Post a Comment