Saturday, 26 March 2016

Wagombea warushiana matusi Marekani



Wagombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican Ted Crus na Donald Trump walirushiana cheche za matusi katika mjadala

Wagombeaji wawili wa Urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamegombana vikali na kurushiana matusi juu ya wake zao.
Seneta wa Texas, Ted Cruz, amemlaumu mpinzani wake, mfanyabiashara Donald Trump kwa kuzusha uvumi kuwa yeye alikuwa mzinifu na kumdanganya mkewe, Heidi.
Bwana Cruz alisema uvumi huo ni takataka na akasema kuwa anaelewa kuwa uvumi ulianzishwa na Bwana Trump ambaye alisema hastahili kuwa Rais.
Bwana Trump alisisitza kuwa hakuhusika vyo vyote na uvumi huo.
Mapema juma hili, Bwana Trump alimlaumu Seneta Cruz kwa kuweka picha za mkewe, Melania, akiwa uchi kwenye mtandao ili kumharibia sifa.

No comments:

Post a Comment