Timu ya taifa ya Romania imekuja na wazo la kuwasaidia watoto wa nchi hiyo kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye somo la Hesabu baada ya kuchapisha jezi zilizobeba maswali ya hesabu mgongoni wakati wakiwa mazoezini.
Nchi hiyo inakiwango kibaya kwenye umoja wa Ulaya kutokana na watoto kuacha masomomo, takribani asilimia 18 (18%) ya watoto wamekuwa wakiacha shule.
“Hisabati na mpira wa miguu vimekuwa havishirikishwi”, amesema Rais wa shirikisho la soka la Romania Razvan Burleanu.
Kutokana na project hiyo, watoto watajifuna kanuni za mchezo wa soka pia watakuwa na fursa ya kutumia mbinu mpya za kuvutia kwa mara ya kwanza inchini humo kujifunza somo la Hisabati.
Mchezo wa kirafiki kati ya Romania dhidi ya Hispania haukusababisha tatizo lolote kwa wanahisabati kutokana na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
No comments:
Post a Comment