Tuesday, 29 March 2016

El Clasico: Madrid hupoteza mechi vs Barca ambazo huwaanzisha pamoja BBC

Real-Madrid-trio-BBC-has-scored-in-2015-only-12-goals



Real Madrid mara zote wamekuwa wakipoteza mechi zao dhidi ya Barcelona wakati Bale, Cristiano na Karim Benzema wanapoanza katika kikosi cha Real Madrid katika mechi vs The Blaugrana.
Hii imejitokeza mara 3 ambapo BBC walianza pamoja katika kikosi cha Madrid dhidi ya mahasimu wao. Kwa kifupi tangu Gareth Bale alipojiunga na Madrid, Los Blancos wamefanikiwa kuifunga mara 2 tu Barcelona: katika fainali ya Copa Del REY 2014 na msimu uliopita @Santiago Bernabeu. Cristiano aliukosa mchezo wa kombe la mfalme na Bale aliukosa mchezo wa ligi kutokana na majeruhi.
Katika misimu miwili na nusu iliyopita wameshinda mechi 2 na kupoteza mmoja bila uwepo wa ukamilifu wa BBC  kuanza pamoja. Mechi ya kwanza ya Bale dhidi ya Barcelona ilikuwa mnamo October 23, 2013. Carlo Ancelotti aliamua kumuacha kwenye benchi Benzema na baadae akamtoa na kumuingiza Bale dakika ya 60. Madrid wakafungwa 2-1.1459189049_436705_1459191951_sumario_normal March 2014 Barça walienda Bernabeu katika mchezo ambao Bale, Benzema na Cristiano wote walianza pamoja katika kikosi cha Madrid – matokeo ya mwisho ya mchezo Madrid wakapoteza kwa 3-4. Madrid wakarudisha kisasi kwa ushindi wa fainali ya Spanish Cup katika dimba la Mestalla – mchezo ambao Cristiano hakucheza na Gareth Bale alifanikisha ushindi wa timu yake kwa kiasi kikubwa.
Msimu uliopita timu hizi zilikutana mara mbili – Madrid walishinda 3-1 katika mchezo wa kwanza, siku ambayo Bale alikosa mchezo huo kutokana na majeruhi. Tangu ushindi huo, mechi mbili za Clasico zimefanyika huku BBC wakianza kwenye mechi zote. Madrid wakafungwa 2-1 katika El Clasico ya mwisho ya Carlo Ancelotti na mechi ya msimu huu ya kwanza kikosi cha Luis Enrique kiliifumua 0-4 Madrid nyumbani @Santiago Bernabeu chini ya uongozi wa Rafa Benitez.
Barcelona VS Real MadridWasiwasi mkubwa kwa Zidane kuwaanzisha BBC kwa pamoja ni kuwaruhusu Barca kutawala kwenye safu ya kiungo na huku safu ya ulinzi ikiwa na uwazi. Katika mechi zote ambazo Madrid walianza na BBC – tofauti ya magoli imekuwa magoli 3. Jumamosi ijayo kila kitu kitategemea na mbinu za kocha Zidane kuwaanzisha Bale, Benzema na Cristiano  katika kikosi cha Madrid ambao wana kumbukumbu ya kupokea kipigo cha 4-0 nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment