Siku 4 kabla ya dunia ya wapenda soka kushuhudia mtanange wa
wapinzani wa jadi wa soka la Hispania – FC Barcelona vs Real Madrid –
nitakuwa nakuletea taarifa muhimu kila siku mpaka siku ya mchezo huo.
Leo
tuangalie historia – takwimu zinaonyesha Barcelona huwa wanapata taabu
sana kupata matokeo dhidi ya Los Blancos wakati wanapokuwa na faida ya
kuongoza ligi kwa pointi nyingi mbele wa wapinzani wao. Barca wanapokuwa
na uongozi wa zaidi ya pointi 9 mbele ya Madrid, historia inaonyesha
huwa wanapata taabu kupata pointi mbele ya Madrid.
Ingawa makampuni mengi ya kamari na wadau wengi wa soka wanaipa nafasi
ya Barca kuibuka na ushindi, historia inatupa picha tofauti ya matokeo.
Na kama matokeo ya siku za nyuma ni ya kuyaangalia kuelekea mchezo huu –
pale Wakatalunya wanapokuwa wanaongoza ligi mbele ya Madrid kwa pointi 9
au zaidi basi mchezo unaofuatia dhidi ya Los Blancos huishia kwa Barca
kufungwa au kutoa sare.
Barca kwa sasa wanaongoza ligi kwa pointi 10 mbele ya Madrid –
Atletico wanashika nafasi ya pili na Madrid wakishika nafasi ya 3 –
katika El Clasico tatu zilizopita ambazo Barca alikuwa anaongoza ligi
kwa tofauti ya pointi hizi basi matokeo huwa hayawi upande wao.
Msimu wa 2012-13 | Pengo la pointi 14 | Real Madrid 2-1 Barcelona
Hii mechi ilikuja wakati kukiwa na pengo kubwa zaidi la pointi baina ya
wapinzani hawa kuelekea El Clasico. Walikutana mnamo Mei 24 katika dimba
la Bernabeu. Kikosi cha Barca chini Tito Vilanova/Roura kilifungwa 2-1,
Karim Benzema na Ramos wakifunga magoli ya ushindi, mchezo ambao
Ronaldo alianzia benchi.
Kumbukumbu nyingine ya mchezo huu ni adhabu ya kadi nyekundu kwa
golikipa Victor Valdes baada ya filimbi ya mwisho kwa kumwambia refa
Perez Lasa “You bottled it, you’re shameless”
Msimu 2005-2006 | 11 points | Real Madrid 1-1 Barcelona
Huku ikiwa imebaki michezo 8 kabla ya ligi kumalizika, kikosi cha
Frank Rijkaard cha Barca walikutana na Madrid @CampNou wakiwa na pointi
11 zaidi kwenye ligi. Florentino Perez alikuwa ameondoka kwenye kiti cha
urais mwezi mmoja nyuma na klabu ikawa kwenye kipindi cha mpito – Lopez
Caro akiliongoza benchi na Fernando Martin akikaimu kiti cha urais.
Pamoja na matatizo waliyokuwa wanapitia Real Madrid, lakini bado
walifanikiwa kuondoka na pointi moja – huku mechi ikajaa malalamiko kwa
refa aliyetoa penati ya utata kwa Barca huku akikataa ya wazi kabisa
kwa Madrid. Robert Carlos alitolewa kwa kadi nyekundu. Lakini goli la
kusawazisha la Ronaldo De Lima likaufanya mchezo uwe sare baada ya goli
la penati la Ronaldinho.
Msimu 1990-91 | 13 points | Real Madrid 1-0 Barcelona
Hakuna maelezo mengi kuhusiana na story ya mchezo huu ambao ulichezwa
huku bingwa akiwa kashafahamika. Barcelona tayari walishakuwa mabingwa
na Atletico akishika nafasi ya pili. Barcelona hii ndio ile ya Johan
Cruyff ‘The Dream Team’ – na inakumbukwa kwamba mdachi huyo alisema
alikuwa na furaha kuona timu yake ikipoteza mbele ya Madrid kila mwaka
ili mradi tu wao wawe mabingwa. Akisema suala la heshima anayopewa
bingwa ‘Guard of Honour’ kabla ya mchezo lilikuwa jambo zuri.
Aldana ndio alifunga goli pekee kwenye mchezo huo huku Zubizarreta
akiokoa penati ya Butragueno ambaye alimaliza akiwa mfungaji bora msimu
huo.
Ushindi wa kwa Barcelona wikiendi ijayo utaweka rekodi mpya na pia
utawapa uongozi wa pointi 13 mbele ya wapinzani wao – ushindi kwa Madrid
utarejesha matumaini ya kusbinda ubingwa kama Barca ataendelea
kuteleza.
No comments:
Post a Comment