Tuesday, 29 March 2016

KIJANA WA NIGERIA MWENYE ULEMAVU, ATIMIZA NDOTO YAKE YA KUKUTANA NA JOHN OBI MIKEL (Video)

Abubakar 1


Kipande cha vieo kilichorekodiwa wakati timu ya taifa ya Nigeria kikifanya mazoezi wiki hii kimemuonesha kiungo wa Chelsea John Obi Mikel akipiga story na kijana mwenye ulemavu wa miguu kitu ambacho kiliwavutia mashabiki wa The Super Eagle waliokuwa wakishuhudia mazoezi ya timu yao ya taifa kulekea mhezo wao wa marudiano dhidi ya Misri.
Abubakar Haruna Gurugu ni kijana mwenye miaka 15 ambaye hawezi kutembea kutokana na ulemavu wake wa miguu, hivyo kijana huyo ambaye ni shabiki wa mkubwa wa Super Eagles hutumia mikono yake na miguu kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Abubakar 2
Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com, striker wa Watford Odion Ighalo ndiyo alikuwa wakwanza kumtilia maanani kijana huyo.
“Alikuwa ni mshambuliaji Odion Ighalo ambaye alianza kumpa kipaumbele Abubakar kisha kijana huyo akaelekea kwa nahodha wa Nigeria John Obi Mikel. Mikel na Abubakar walizungumza kwa takribani dakika tano kuhusu mchezo wa Ijumaa pamoja na mambo mengine mengin wakiwa wamekaa kwenye njia za kukimbilia za uwanjani”.
Abubakar
Abubakar Haruna Gurugu alizungumza na mtandao mmoja wa soka kuhusu vitu alivyozungumza na baadhi ya wachezaji wa Nigeria.
“Sikufurahishwa na matokeo ya sare. Misri wanawezaje kutoka sare dhidi ya Nigeria kwenye uwanja wa Kaduna!”.
Taarifa zinadai kwamba, Ighalo alibadilishana namba za simu za kijana huyo huku Mikel akiahidi kutoa msaada kwa familia ya Abubakar.

No comments:

Post a Comment