Rais
Mstaafu wa awamu ya nne na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika
Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkaribisha Waziri wa
Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria Mheshimiwa Abdelkader
Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini
Tunisia.
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika
Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Waziri wa
Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria Mheshimiwa Abdelkader
Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini
Tunisia.
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika
Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiagana na Waziri wa
Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria Mheshimiwa Abdelkader
Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini
Tunisia.
…………………………………………………………………………………….
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika wa
Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya, amewasili jana Jijini Tunis nchini
Tunisia kushiriki Mkutano wa 8 wa Nchi majirani wa Libya.
Mkutano huo umeitishwa na Serikali
ya Tunisia, na ni muendelezo wa jitihada za nchi majirani kusaidia
kuleta hali ya amani na usalama nchini Libya.
Rais Mstaafu Kikwete amewasili
Tunis akitokea Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya
Bunge la Kuandika Katiba ya Libya.
Akiwa Jijini Tunis, Jana tarehe 22
Machi, 2016 Dkt. Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Masuala ya
Maghreb, nchi za Kiarabu na Afrika, wa Algeria Mheshimiwa Abdelkader
Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake.
Katika mazungumzo hayo, Waziri
Messaleh amempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa
Nchi wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya. Amemueleza hali ya
usalama na kisiasa ya Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya namna bora
ya utatuzi wa mgogoro huo, na akamhakikishia ushirikiano wa Serikali ya
Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa Afrika.
Kwa upande wake, Rais Mstaafu
Kikwete amemshukuru Waziri Abdelkader Messaleh kwa maelezo yake na
ushirikiano aliomuahidi na akamueleza matumaini yake ya kupatikana kwa
suluhu ya mgogoro huo hasa ikizingatiwa kuwa nchi jirani na Libya na
Umoja wa Afrika zitashirikiana na wadau wote kuhakikisha mgogoro huo
unatatuliwa.
Rais Mstaafu Kikwete amesisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.
Katika ziara yake nchini Tunisia,
mbali na kuhudhuria Mkutano wa 8 wa nchi jirani na Libya, Rais Mstaafu
Kikwete anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu Mteule na Mwenyekiti wa
Baraza la Utawala la Libya, (Presidency Council) Mheshimiwa Fayez
Al-Sarraj, wadau wengine wa Libya pamoja na kutembelea Ofisi ya Ujumbe
wa Umoja wa Afrika kwa Libya iliyoko jijini Tunis.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 25 Machi, 2016.
Imetolewa; Ofisi ya Rais Mstaafu.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Tunis
22 Machi, 2016
No comments:
Post a Comment