Aliyekuwa
Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam kupitia tiketi ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Yenga Yusuph alipokuwa akiomba kura kwa
wajumbe walioshiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Meya leo jijini
Dar es salaam.
Baadhi
ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki zoezi la kupiga
kura ya kumchagua Meya wa Jiji leo Dar es Salaam (Kushoto) ni Mbunge wa
Jimbo la Ilala Mhe. Iddy Azzan Zungu na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la
Segerea Mhe. Bonnah Kaluwa.
Baadhi ya wapiga kura waliohudhuria uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Leo 22/03/2016 wakifuatilia uchaguzi huo.
Baadhi
ya Maafisa kutoka Ofisi za Jiji Dar es Salaam wakifuatilia Uchaguzi
wa Meya uliyofanyika leo (kwa kwanza kulia) ni Afisa Sheria Mkuu
Jumanne Mtinangi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Mhe. Agustine Mahiga
akizungumza na aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji kupitia Chama
cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yenga Yusuph.
Mbunge
wa Viti Maalum Kinondoni kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Mhe. Suzan Lyimo (kushoto) pamoja na Mbunge wa jimbo la Kawe
Mhe. Halima Mdee (CHADEMA) wakifuatilia zoezi la Upigaji kura wa
kumchagua wa Meya leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward
Lowasa akimpongeza mshindi wa nafasi ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam
Mhe. Isaya Chacha mara baada ya kutangazwa mshindi leo jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Jiji la Dar es
Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Mhe. Isaya Chacha Diwani wa Kata ya
Vijibweni (CHADEMA) kutoka Manispaa ya Temeke kuwa Meya Mpya wa Jiji
hilo.
Kaimu Mkurugenzi huyo alimtangaza
Isaya kuwa mshindi mara baada ya uchaguzi huo kufanyika leo jijini Dar
es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67 wakati
kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.
“Tunawashuruku wapiga kura wote
mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza
kufanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili” alisema Bi Yohana.
Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha
Meya wa Jiji Mhe. Chacha aliwashukuru wapiga kura wake wa kata ya
Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake
kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.
“Nimejipanga kuleta maendeleo
katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji
letu na nitahakikisha wananchi wote maskini wanafaidika na mapato ya
jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.
Aidha, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa
Bw.Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa
ushindi wa kiti hicho cha Meya ni lazima uchukuliwe na CHADEMA sababu
madiwani wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.
No comments:
Post a Comment