Monday, 21 March 2016

Obama alivyoweka Historia ya mahusiano ya Marekani na Cuba

Baada ya kutokuwa na uhusiano mzuri kati ya Marekani na jirani yake Cuba kwa muda mrefu, March 20 2016 Rais Barack Obama amefanya ziara ya siku 3 inayolenga kurekebisha  uhusiano wao na Cuba huku Cuba inataka kuondolewa zaidi vikwazo vyote vya kiuchumi na Marekani.
Rais Barack Obama amewasili na Air Force one Jumapili  ikiwa ni Rais wa kwanza kutembelea Cuba tangu Calvin Coolidge ambaye alitembelea wakati wa vita mwaka 1928. 
Rais Barack Obama ametembelea kwenye mji wa kale wa Havana na pia alizungumza na wafanyakazi wa ubalozi mpya wa Marekani na amesema…>>>imekuwa ni miaka 88 toka Rais wa Marekani kufika hapa Cuba, ni maajabu kuwa hapa. Mwaka 1928 Rais Coolidge alikuja kwenye vita, ilimchukua  siku tatu kuwa hapa, imenichuka masaa matatu tu kuwa hapa, kwa mara ya kwanza Air force one imetua Cuba na hii ni hatua ya kwanza na  fursa ya kihstoria kushirikiana na watu wa Cuba‘:-Barack Obama

.
Rais wa Marekani Barack Obama akikwepa dimbwi la maji wakati alipotembelea mji wa kale Havana.

.
.
.

No comments:

Post a Comment