Monday, 21 March 2016

Eti hii ndio itakuwa mechi yake ya kwanza Pep Guardiola atakapojiunga na Man City

Kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya FC Bayern Munich akimalizia mkataba wake, kabla ya kujiunga na Man City mwishoni mwa msimu Pepe Guardiola, tayari mechi yake ya kwanza akijiunga na Man City kuna tetesi kuwa imejulikana.
Pepe Guardiola anatajwa kuwa na tetesi mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Man United ambayo inadaiwa kuwa kwa wakati huo itakuwa ikifundishwa na Jose Mourinho, ila itakuwa ni michuano ya maandalizi ya msimu ‘International Champions Cup’ itakayofanyika Beijing China.
Jose-Mourinho-and-Josep-Guardiola
Kutoka kushoto ni Jose Mourinho na Pep Guardiola
Hata hivyo ukweli wa kukutana au kutokukutana utajulikana wiki hii, kwa sasa mashabiki wa Man United wanaimani kuwa Louis van Gaal atafukuzwa mwishoni mwa msimu na Mourinho atajiunga nao, wakati Man City wao walithibitisha kuwa tayari walisaini mkataba na Guardiola.

No comments:

Post a Comment