Sunday, 20 March 2016

NIMEKUWEKEA MATOKEO YA LIGI YA ENGLAND HAPA YATAZAME MAN CITY HOI WAPIGWA MOJA NA MAN UNITED




Jumapili Machi 20
Newcastle 1 Sunderland 1          
Southampton 3 Liverpool 2         
Man City 0 Man United 1            
Tottenham 3 Bournemouth 0


 


TINEJA Marcus Rashford Leo aliifungia Manchester United Bao pekee na la ushindi kwenye Dabi ya Jiji la Manchester walipowatungua Manchester City 1-0 na kuweka hai matumaini yao ya kumaliza ndani ya 4 Bora.
Bao la Rashford lilifungwa Dakika ya 15 baada kupokea Pasi murua ya Juan Mata na kumpiga chenga Sentahafu wa City Demichelis na kupiga shuti kifundi kumzidi akili Kipa Joe Hart.
Bao hilo limeweka Rekodi mpya huko England kwa Rashford, ambae ana Miaka 18, kufunga Bao kwenye Dabi akiwa Kijana mdogo kabisa.
Man United wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi sawa na Timu ya 5 West Ham ambao wamewazidi Bao 1 tu huku City wakiwa Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 tu mbele.
VIKOSI:
Man City: Hart; Sagna, Demichelis, Mangala, Clichy; Toure, Fernandinho; Jesus Navas, Silva, Sterling; Aguero
Akiba: Zabaleta, Fernando, Kolarov, Caballero, Bony, Iheanacho, Manu Garcia.
Man United:De Gea; Darmian, Smalling, Blind, Rojo; Carrick, Schneiderlin; Lingard, Mata, Martial; Rashford
AKIBA: Depay, Januzaj, Romero, Valencia, Fellaini,Schweinsteiger, Fosu-Mensah.
REFA: Michael Oliver
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 2
1445 Aston Villa v Chelsea
1700 Arsenal v Watford              
1700 Bournemouth v Man City    
1700 Norwich v Newcastle          
1700 Stoke v Swansea                
1700 Sunderland v West Brom    
1700 West Ham v Crystal Palace  
1930 Liverpool v Tottenham                  
Jumapili Aprili 3
1530 Leicester v Southampton    
1800 Man United v Everton        

No comments:

Post a Comment