Katika mitandao ya kijamii Jumamosi iliyopita kulisambaa picha za rapa Chidi Benz ambazo zinamuonyesha jinsi alivyokonda na kupoteza ule mwili wake wa kuvutia aliokuwa nao zamani.
Mkali
huyo wa wimbo Dar es Salaam Stand Up, anakubalika na vijana wengi
kutokana na uwezo wake wa kuandika pamoja na kuchana. Lakini miaka ya
hivi karibuni alianza kubadilika baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya
madawa ya kulevya.
Oktoba
24 mwaka 2014, Chidi alikamatwa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa
Ndege wa JK Nyerere wakati akielekea jijini Mbeya kwa ajili ya show.
Lakini kesi hiyo ilimalizika miezi michache baadaye baada ya kuamriwa na
mahakama kulipa faini.
Tukio
hilo liliwafanya wasanii mbalimbali kuzungumzia hali hiyo huku
wakimshauri kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya. Ray C ambaye ni
mmoja kati ya waathirika janga hilo ambaye kwa sasa yupo kwenye tiba ya
methadone, aliamua kumshauri Chid Benz.
“Pole
kaka yangu Chidi Benz. Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado
haujalitafutia jibu la kutatua tatizo lako. Mimi ni dada yako
natumeshafanya kazi pamoja, tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na
niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu
kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na
kunitandika nalo nyumbani,” aliandika Ray C kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Hata
hivyo Chidi Benz aliendelea na harakati zake huku akijinadi katika
vyombo vya bahari kwamba tayari ameshaachana na matumizi ya madawa ya
kulevya. Lakini watu wake wa karibu pamoja na marafiki zake walikuwa
wanadai kwamba bado hajaacha.
Lakini Jumamosi hii akiwa katika kipindi cha Da Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chidi amelionekana amechoka zaidi huku akiowamba wadau mbalimbali kumsaidia.
Lakini Jumamosi hii akiwa katika kipindi cha Da Weekend Chart Show cha Clouds TV, Chidi amelionekana amechoka zaidi huku akiowamba wadau mbalimbali kumsaidia.
“Matatizo
yangu na stress zangu ambazo niko nazo zinanisababishia mwili wangu
unapungua kwasababu siko okay, siko poa, siko sawa yaani,” alisema.
Mmoja
kati ya wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop, Afande Selle, alionyesha
kusikitishwa na jinsi madawa ya kulevya yanavyomaliza nguvu kazi ya
taifa.
“Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,” alisema Afande Selle.
“Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? Anayasambaza nani mitaaani kote mitaani? Madawa ya kulevya hayaleti maendeleoooo,madawa ya kulevya yanaua masela leooooo,” alisema Afande Selle.
Pia
wadau mbalimbali wamewataka watu pamoja na wasanii wenzake kumsaidia
huku Arnold Kayanda, mtangazaji wa BBC Swahili akisema amelipokea kwa
masikitiko suala hilo.
“Kama
picha hii ni rafiki yangu Chidi Benz kama nilivyotaarifiwa, kwa hisani
yenu wote naomba kila mtu kwa nafasi yake amsaidie. Mimi niko mbali
lakini nikirudi nitakutana naye,” alisema.
Licha
ya wadau mbalimbali kutaka asaidiwe lakini bado tunaona hakuna msaada
wa haraka ambao mpaka sasa umechukuliwa ili kumuokoa Chidi Benz.
Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.
Serikali ya Magufuli ni sikivu sana, bila shaka kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri kijana mpenda sanaa, Nape Moses Nnauye ataliangalia suala hili.
No comments:
Post a Comment