Aliyekuwa Mgombea
Urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Oktoba 25, mwaka jana, ambaye
pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad,
amesema hatma ya Wazanzibar iko mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Maalim Seif alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa ni nini hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika jana.
“Mimi
sijui, waulizeni CCM wao ndiyo wametengeneza hali hii, wao ndiyo
wamekusudia na wanajua wanaipeleka wapi nchi hii, watasema wao,” alisisitiza Maalim Seif.
Aliyasema
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa
na Vijana wa Baraza la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema-Bavicha
jijini Dar es Salaam jana kumjulia hali.
Baada
ya kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana, hali ya kisiasa ya
Zanzibar imedaiwa kuwa tete haswa kutokana na CUF kudai hawatambui
kufutwa kwa uchaguzi huo msimamo wao wakitaka mshindi atangazwe.
Maalim
Seif alisema CCM wanafahamu wazi kwamba mshindi aliyeshinda katika
uchaguzi wa wa Okotoba 25, ni nani, lakini wameamua kufanya hivyo na
kuifikisha Zanzibar hapo ilipo sasa.
Alisema
miaka mitano iliyopita kulikuwa kumepatikana maridhiano Zanzibar na
walikuwa wameanza kwenda vizuri, lakini kinachoonekana hivi sasa
wameanza kuwarudisha nyuma kwa kuvuruga tena maridhiano hayo na kuanza
kuleta uhasama.
“Hapo
nyuma kulikuwa na uhasama wa kisiasa Zanzibar halafu ukaisha, lakini
hivi sasa wanaurudisha, CCM ndiyo wameamua iwe hivyo,” alisema Maalim Seif.
Kadhalika,
Maalim Seif alisema anaamini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
(Zec), Jecha Salim Jecha, ametumwa kuitafutia kura CCM.
“Jecha
ametumwa kuitafutia kura CCM, lakini ijulikane kwamba hata wafanye
vyovyote watakavyofanya, Wanzanzibari ndani ya mioyo yao, wanafahamu
Rais wao ni mimi,” alisema Maalim Seif na kuongeza:
“Kinachotokea
Zanzibar ni mipango iliyopangwa na CCM ambao pamoja na kwamba
wanamfahamu mshindi ni nani katika uchaguzi wa mwaka jana, lakini
wameamua kufanya hicho wanachofanya hivi sasa.”
Aidha, alisema kwa sasa hataki kusema chochote, isipokuwa anasubiri Rais atangazwe.
Maalim
Seif yuko jijini Dar es Saalam kwa mapumziko mafupi baada ya kuugua na
kuruhusiwa kutoka hospitali zaidi ya wiki moja iliyopita.
No comments:
Post a Comment