Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa
Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka
Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati
wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20
Machi, 2016
Habari
hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao
Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya
Ulinzi wa nchi yetu.
Hivyo
hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani
humo tangu awali. Taarifa hizo zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya
kujenga hofu kwa Wananchi.
JWTZ
linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na
wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu, kwani wakati
wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.
No comments:
Post a Comment