Mahakama ya
kimataifa ya makosa ya jinai -ICC yenye makao yake makuu huko Hague
nchini Uholanzi, imempata na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita
aliyekuwa makamu wa rais wa Congo Jean-Pierre Bemba.
Bwana Bemba
alishindwa kuishawishi mahakama kuwa alishindwa kudhibiti kundi la
wapiganaji wasiwauwe watu, kuwabaka wanawake na wasichana katika taifa
jirani la Afrika ya kati.Mnamo mwaka 2002-2003 aliwatuma maelfu ya wanajeshi wake hadi nchi hiyo ili kusaidia kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya rais wa taifa hilo wakati huo.
Bwana Bemba amekanusha makosa hayo wakili wake akisema kuwa hakuwa na uwezo wa kuwadhibiti wapiganaji wake.
Mawakili wake wanasema kuwa hakuwa na uwezo wa kulidhibiti kikosi chake cha kivita.
Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo ya ICC kuangazia kesi dhidi ya dhuluma za kingono kama silaha ya vita.
Majaji wanasema kuwa japo Bemba alikuwa amiri jeshi mkuu wa kundi hilo alishindwa kabisa kuwakanya wasitekeleze makosa ya uhalifu wa kivita.
No comments:
Post a Comment