Thursday, 17 March 2016

HAYA NI MANENO YA WENGER BAADA YA KUFUNGWA NA BACA

Image result for WENGER

Arsene Wenger amesisitiza Arsenal itaokoa Msimu wao uliosambaratika kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England.
Jumatano Usiku, Arsenal walitupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kuchapwa 3-1 na Barcelona huko Nou Camp baada ya pia kupigwa 2-0 kwenye Mechi ya kwanza huko Emirates na kutolewa kwa jumla ya Bao 5-1.
Pigo hilo linafuatia lile la Wikiendi iliyopita walipopigwa 2-1 na Watford na kutupwa nje ya FA CUP ambayo wao ndio walikuwa Mabingwa kwa Misimu Miwili iliyopita.
Hivi sasa Arsenal wako Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City lakini kikwazo hicho Wenger hakioni.
Alipohojiwa mara baada ya kutwangwa na Barca kama bado ana matumaini ya Ubingwa England, Wenger alijibu: “Nadhani ndio. Nimefurahia uchezaji wetu na Barca. Ila nimehuzunishwa na matokeo lakini tumecheza na Timu yenye Mastraika Watatu bora ambao sijapata kuwaona! Ligi Kuu iko nyeupe kupita Watu wanavyofikiria!”
Kwenye kipigo hicho cha 3-1, Bao za Barca zilifungwa na Neymar, Suarez na Messi, Mastraika ambao sasa kwa pamoja wanaitwa MSN na Wenger ameungama: “Barcelona wana Wachezaji Wawili au Watatu ambao hubadilisha maisha ya kawaida kuwa Sanaa!”

No comments:

Post a Comment