Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram wamewateka nyara wanawake 16 katika
eneo la mashambani, Kaskazini Mashariki mwa Jimbo la Adamawa.
Vyanzo
vya habari vilisema wanawake hao walitekwa msituni, walipokuwa
wakitafuta kuni na wengine walikuwa wakivua samaki kando ya mto.
Wanawake hao hadi sasa hawafahamiki mahali walipohifadhiwa na watekaji.
Kundi
hilo lililoenea nchini humo, limekuwa likijihusisha na vitendo vya
utekaji wa mara kwa mara. Awali, liliwateka wasichana ambao ni wanafunzi
zaidi ya 200 ambao mpaka sasa hawajapatikana.
Wakati huohuo,
Jeshi la Nigeria limewakomboa zaidi ya watu 800, waliokuwa wakishikiliwa
na kundi hilo katika vijiji kadhaa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Mateka
wengine walikombolewa katika Jimbo la Borno, huku 520 wakikombolewa
katika Kijiji cha Kisuma, baada ya mapambano kati ya wanajeshi hao na
wapiganaji wa kundi hilo, mateka wengine 309 waliokolewa katika vijiji
vingine 11 vinavyodhibitiwa na kundi hilo.
Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari alipokuwa anaingia madarakani alisema atahakikisha anapambana na kundi hilo
No comments:
Post a Comment