WATU
saba wamekufa na wengine 10 k u j e r u h i w a baada ya gari
walilokuwa wanasafiri nalo aina ya Mitsubishi Fuso kupasuka tairi la
mbele na kugonga kingo za barabara katika barabara kuu ya
Igunga-Singida.
Wengi wao walikuwa wafanyabiashara ya samaki waliokuwa wakitokea Igunga kwenda kijiji cha Loya wilayani Uyui, Tabora.
Kutokea
kwa ajali na vifo hivyo kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa
Tabora, Khamis Selemani Issah aliyesema ilitokea majira ya saa tatu
usiku katika kijiji cha Nanga, kata ya Nanga wilaya ya Igunga.
Alisema
lori hilo lenye namba za usajili T 124 ACS lilibeba abiria wengi
kinyume na sheria za usafirishaji wa abiria na kuongeza kuwa hatua kali
zitachukuliwa kwa watakaobanika kubeba abiria katika magari ya mizigo.
Mara
baada ya ajali hiyo, dereva wake aliyetajwa kuwa ni Joseph Masali
alitoweka eneo la tukio na jeshi la polisi linamtafuta aweze kujibu
tuhumu zinazomkabili kuhusiana na ajali hiyo.
Kamanda
huyo aliendelea kusema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva
kutokana na mwendo kasi pamoja na pia kwa kuvunja sheria ya kubeba
abiria kwa gari la mizigo.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Abdallah Ombeni alipokea
majeruhi 11 na miili 6 katika hospital hiyo huku majeruhi mmoja
alisafirishwa katika Hospital ya Rufaa ya Nkinga kwa matibabu zaidi
kutokana na hali yake kuwa mbaya, hata hivyo alifariki dunia akiwa
njiani.
Amewataja
waliokufa kuwa ni Masesa Sagalali, Omar Rajabu, Shaaban Ibrahim,
Sagalali Maige, Selestine Lipande, Juma Iddi na mwingine aliyetambulika
kwa jina mmoja la James. Juma Hassan, mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo
alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.
No comments:
Post a Comment