Thursday, 18 February 2016

Uchaguzi Mkuu Uganda: Mitandao Ya Kijamii Imefungwa Na Miamala Ya Simu Imezuiliwa


Waganda leo wanapiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge, unaofanyika huku kukiwa na malalamiko ya masanduku ya kupigia kura kufikakwa  kuchelewa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na kufungwa kwa mitandao ya kijamii.

Leo asubuhi asubuhi misururu mirefu ya watu ilionekana katika vituo vya kupigia kura mjini Kampala ambapo zoezi la kupiga kura lilianza kwa kuchelewa kwa zaidi ya saa moja na nusu kufuatia maafisa wa uchaguzi kuendelea na matayarisho ya vifaa vya kupigia kura.

Zoezi hilo la upigaji kura linatazamiwa kukamilika saa kumi jioni saa .Bado hapajakuwa na taarifa zozote iwapo zoezi hilo litarefushwa kufuatia baadhi ya vituo kuanza shughuli hiyo kwa kuchelewa.

Mawasiliano ya yamitandao ya jamii yafungwa
Huku hayo yakiarifiwa mdhibiti wa mawasiliano wa serikali ametangaza kufungwa kwa mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter na kufunga mifumo ya kutuma pesa kupitia njia ya simu. 

Kwa majibu wa mkuu wa kamisheni ya mawasiliano nchini Uganda Godfrey Mutabaazi aliyezungumza na kituo cha radio cha CBS, hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.

Msemaji wa wizara ya nje ya Marekani Mark Toner amesema Washington ina wasiwasi kuwa vikwazo hivyo vya mawasiliano huenda vikasababisha mivutano zaidi katika nchi ambayo tayari inakumbwa na joto kali la uchaguzi.

Kwa upande mwingine wanaharakati wa haki za binaadamu wameelezea wasiwasi wao pia juu ya madai ya kuundwa kwa makundi ya vijana wenye silaha wanaohusishwa na vyama pamoja na wanasiasa mbali mbali kwa ajili ya kulinda maslahi ya vyama vyao kwenye uchaguzi huu.

Museveni aliye na miaka 71 aliyechukua madaraka kwa mara ya kwanza nchini Uganda mwaka wa 1986 na aliyeshinda uchaguzi mara nne kuanzia mwaka wa 1996, anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wawili kati ya wagombea saba waliopo katika kinyang'anyiro cha urais.

Kizza Besigye, aliye na miaka 59, aliyekuwa daktari wa Museveni ndiye mgombea wa kwanza anayempa tumbo joto Museveni. 

Besigye ameshashindwa mara tatu katika safari yake ya kuwania urais nchini Uganda. Mwingine anayeonekana kutoa ushindani mkali ni Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi aliye na miaka 67.

No comments:

Post a Comment