Wednesday, 13 January 2016

WATUMISHI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOLO WAPIGWA MARUFUKU KUISHI NJE NA VITUO VYAO VYA KAZI



 Image result for VENANCE MWAMOTO AKIWA KWENYE KIKAO

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, imepiga marufuku watumishi wake kuishi nje ya vituo vyao vya kazi kwa madai ya kufuata familia zao.

Agizo hilo limekuja kufuatia mbunge wa jimbo la kilolo Venance Mwamoto kuhoji katika kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya (DCC), kutaka kujua sababu ya baadhi ya watumishi kukosa vitambulisho pindi wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi 

Akitoa agizo hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bi. Rukia Muwango, amesema wapo baadhi ya watumishi wanafanya kazi Wilaya ya Kilolo na kuishi nje ya Wilaya ya Kilolo jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kazi.

Bi.Muwango ametaka kila mtumishi wa Wilaya hiyo kuishi katika Kituo chake cha kazi na si vinginevyo, na kuwa wapo baadhi ya watumishi ambao wamehamishiwa katika halmashauri hiyo na wamekuwa wakifanya kazi ndani ya Wilaya, ila wanaishi nje ya Wilaya hiyo kwa kisingizio cha kufuata familia zao.

Wakati huo huo Wilaya ya Kilolo imepokea Jumla ya tani 80 za mahindi ya chakula cha msaada ambayo ni tani 8 kutoka ofisi ya Waziri mkuu kitengo cha maafa toka septemba 25 mwaka jana  na kuwa tani 8 zilitolewa bure kwa watu wasio na uwezo wa kiuchumi na tani 72 zikiuzwa kwa walengwa.

No comments:

Post a Comment