WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amemtembelea na kuampa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia Nyerere.
Akizungumza
na mama Maria alipomtembelea nyumbani kwake jana(Jumanne, Januari
12,2016), Msasani jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu ametoa pole kwa
Mama Maria Nyerere pamoja na familia na kuwaomba waendelee kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na mpendwa
wao.
“Kipindi
hiki ni kigumu, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo, pia
tutajumuika nanyi katika kipindi hichi chote, tuendelee kuwa watulivu na
kumwomba Mungu” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Ndugu
wa marehemu, John Shibuda (aliyewahi kuwa mbunge wa CHADEMA) ameeleza
kutokea kwa msiba huo. Ambapo amesema “Desemba, 19 mwaka huu Leticia
Nyerere alipelekwa nchini Marekani kwa matibabu na alifariki dunia
katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland juzi saa 2
usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Aidha,
Shibuda amemshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kwenda kuipa pole
familia na Serikali kwa namna ambavyo inatoa ushirikiano mzuri kwa
familia.
Naye,
Rose Nyerere amesema familia inaendelea na maaandalizi, hivyo watatoa
taarifa ya baada ya kuandaa utaratibu wa siku ambayo mwili utaletwa
nchini, kuagwa na hatimaye kuzikwa Butiama.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ambaye amelazwa siku kadhaa
zilizopita katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Majaliwa, amesema amefarijika baada ya kumuona Waziri Mkuu huyo
mstaafu akiendelea vizuri na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa
kumpatia matibabu na kumhudumia vizuri. Pamoja na kumpa pole, Waziri
Mkuu amemwombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya
kila siku.
Naye,
Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa
kwa kumtembelea hospitalini hapo, pia ameipongeza Serikali kwa jitihada
mbalimbali inazofanya ili kusaidia wananchi na hatimaye kuiletea nchi
maendeleo.
“Naipongeza
Serikali kwa namna ambavyo inaendelea kutekeleza majukumu yake katika
masuala mbalimbali yenye lengo la kusaidia wananchi” alisema Sumaye.
Waziri
Mkuu Majaliwa, pia amemtembelea na kumjulia hali Balozi Hassan kibelloh
ambaye amelazwa na anaendelea kupatiwa matibabau katika Taasisi ya
Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, JANUARI 13, 2016.
No comments:
Post a Comment