Mchezaji
Mbwana Samatta aliyejishindia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa
wachezaji wa Ndani nchini Nigeria amezawadiwa na serikali kiwanja
kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam na fedha taslimu ambazo kiasi
chake hakijafahamika.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Lukuvi
anayeonekana katika picha katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya
Hyyat Regency jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa
serikali.
Baadhi
ya viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine wengi wa serikali
na wanamichezo.
Mbwana
Samatta aliyekuwa akicheza mpira wa kulipwa katika timu ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayomilikiwa na tajiri wa madini
na aliyewahi kuwa Gavana wa jimbo la Katanga nchini humo Moise Katumbi
anatarajiwa kujiunga na timu ya KRC Genki ya Belgium barani ulaya.
No comments:
Post a Comment