Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke katika mkutano na waandishi wa habari, Mei 30, 2015, Zurich.
Na RFI
Mwezi
mmoja na nusu kabla ya uchaguzi wa rais wa shirikisho la Soka Duniani
(FIFA), vigogo wa shirikisho hilo wanaendelea kukabiliwa na hatua kali.
Namba 2
wa FIFA Jérôme Valcke amefutwa kazi Jumatano hii baada ya kuhusishwa na
mauzo ya tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2014, sehemu nyingine ya mgogoro
mkubwa unaoikabili taasisi kuu ya mpira wa miguu.
Ni kwa
uamuzi wa kamati ya dharura ambapo mkataba wa ajira kati ya FIFA na
Jérôme Valcke, mwenye umri wa miaka 55, na mtu wa karibu wa Joseph
Blatter tangu mwaka 2007, umevunjwa.
"Jérôme
Valcke anaridhishwa na kila kitu kililiyokamilika chini ya utawala wake
wa Katibu mkuu, ambapo Kombe mbili za dunia zikiwa ni miongoni mwa
mafanikio katika historia ya soka, nchini Afrika Kusini na Brazil.
Valcke ana imani kuwa, historia itakumbuka mchango wake kwa mchezo
anaoupenda", amesema mwanasheria wake, raia wa Marekani, Barry Berke
katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la Ufaransa AFP.
Chini ya
mwezi mmoja, shirikisho la Soka Duniani limewapoteza viongozi wake
vigogo watatu, kwani tangu Desemba 21, Sepp Blatter, rais wa FIFA
aliyejiuzulu, na Michel Platini, rais wa shirikisho la Soka Ulaya
(UEFA), walisimamishwa kwa muda wa miaka 8 katika shughuli ya aina
yoyote inayohusiana na mpira wa miguu.
Blatter,
mwenye umri wa miaka 79, na Platini, mwenye umri wa miaka 60,
waliadhibiwa na Mahakama ya ndani ya FIFA kwa kosa la malipo yenye utata
ya Euro milioni 1,8 mwaka 2011 bila kuwa na mkataba wowote. Majaji wa
FIFA waliona hayo kama "matumizi mabaya ya madaraka" na "mgogoro wa
maslahi".
Hivi
karibuni Michel Platini alijiondoa katika kinyan'ganyirio cha kuwania
urais wa FIFA, uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 26 mjini Zurich,
akibaini kwamba hana muda wa kutafuta wapiga kura.
Mpaka
sasa watu watano ndio wanajulikana kama wagombea kwenye wadhifa huo:
mjumbe wa zamani wa FIFA, Jérôme Champagne, Katibu mkuu wa shirikisho la
Soka Ulaya Gianni Infantino, mfanyabiasahra wa Afrika Kusini Tokyo
Sexwale, mwanamfalme wa Jordan Ali na rais wa Shirikisho la Soka barani
Asia Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa
No comments:
Post a Comment