Saturday, 9 January 2016

Serikali ya ahidi kuendelea kutatua kero za wasanii

na1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyevaa batiki) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii mara baada ya kumaliza kikao na Kamati ya wasanii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija-WHUSM
na2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (mwenye shati la batiki) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya wasanii wa Muziki inayofuatilia suala la malipo ya mrabaha kutokana na kazi zao Jijini Dar es Salaam.
na3
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wajumbe wa Kamati ya wasanii wa Muziki inayofuatilia suala la malipo ya mrabaha kutoka kwa vyombo vya habari na miito ya simu. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mungereza leo jijini Dar es Salaam.
na4
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambaye pia ni Kiongozi wa Kamati ya wasanii wa muziki Bw. Nickson Simon kwa jina la kisanii Nikki wa Pili akiwasilisha hoja za kwa niaba ya wasanii wenzake wakati wa kikao baina yao na waheshimiwa Mawaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja Mhe. Nape Moses Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sana Bibi. Leah Kihimbi na kushoto ni msaanii Ditto.
na5
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambaye pia mjumbe wa Kamati ya wasanii wa muziki akichangia mada wakati wa kikao baina yao na waheshimiwa Mawaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja Mhe. Nape Moses Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage leo jijini Dar es Salaam.
na6
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na msanii mkongwe wa muziki wa injili Bw. Cosmas Chidumule mara baada ya kumaliza kikao na Kamati ya wasanii leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment