Mume wa muimbaji Céline Dion, René Angélil amefariki dunia siku ya Alhamisi [January 14] nyumbani kwao Las Vegas baada ya kuugua ugonjwa wa Saratani, Amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
René Angélil alikuwa Meneja wa music ambaye aligundua kipaji cha Céline Dion akiwa na umri wa miaka 12, baadae walifunga ndoa mwaka 1994.
Céline alichukua likizo kutoka kwenye muziki kwa vipindi viwili ili kumuuguza mumewe, Angelil baada ya kupatikana na saratani ya koo mwaka 2000.
No comments:
Post a Comment