Wednesday, 13 January 2016

MATOKEO YA LIGI YA MICHEZO YA JANA

 Image result for premier league image

  Aston Villa 1 Crystal Palace 0    
         
Bournemouth 1 West Ham 3 
              
  Newcastle 3 Man United 3     

 
Man United wameupoteza uongozi wa 2-0 na kutoka Sare 3-3 na Newcastle huko Saint James Park na kuporomoka hadi Nafasi ya 6.
Man United walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 9 kwa Penati ya Wayne Rooney ambayo ilitolewa baada ya Mpira wa Kona kupigwa Kichwa Fellaini na kumgonga Mbemba mkononi.
Bao la pili la Man United lilifungwa na Jesse Lingard kufuatia kaunta ataki iliyoanzia kwa Ander Herrera na kukumkuta Rooney alietoa pasi kwa Lingard na kufunga.
Dakika ya 42 Newcastle walipata Bao baada ya pasi ndefu ya Coloccini kutulizwa kwa Kichwa na Mitrovic na kumkuta Wijnaldum aliefunga vizuri.
Hadi Mapumziko Newcastle 1 Man United 2.
Kipindi cha Pili kilizaa Bao 3 na Mechi kumalizika kwa Sare ya 3-3

MAGOLI:
Newcastle 2
-Georginio Wijnaldum, Dakika ya 42
-Aleksandar Mitrovic 67 [Penati]
-Paul Dummet 90
Man United 3
-Wayne Rooney, Dakika ya 9 [Penati] na 79
-Jesse Lingard 38

Huko Villa Park, Mechi kati ya Aston Villa na Crystal Palace ilimalizika kwa Villa kuifunga Palace 1-0.
Nao Bournemouth, wakiwa Nyumbani, waliongoza 1-0, West Ham na kumaliza wakichapwa 3-1.

No comments:

Post a Comment