Wednesday, 13 January 2016

MATOKEO YA LIGI YA ENGLAND MICHEZO YA JANA USIKU NIMEKUWEKEA


BPL-2015-16-LOGO1
Chelsea 2 West Brom 2          
Man City 0 Everton 0                
Southampton 2 Watford 0                  
Stoke 3 Norwich 1          
Swansea 2 Sunderland 4          
Liverpool 3 Arsenal 3                
Tottenham 0 Leicester 1 

BAO la Dakika ya 90 la Joe Allen limeipa Liverpool Sare ya 3-3 na kuufuta uongozi wa Arsenal wa Pointi wa Ligi Kuu England na sasa kufungana kwa Pointi kileleni na Leicester City BPL-JAN13ambao Jana waliifunga Tottenham 1-0 huko White Hart Lane.
Mara mbili Liverpool, wakicheza kwao Anfield, waliongoza kwa Bao za Roberto Firmino na Arsenal kusawazisha kupitia Aaron Ramsey na Olivier Giroud.
Bao la Dakika ya 55 la Giroud lilipa uongozi Arsenal wa 3-2 lakini Joe Allen akaisawazishia Liverpool Dakika ya 90 na kuwapa Sare ya 1-1.
Huko White Hart Lane, Bao la Dakika ya 83 la Beki Robert Huth limewapa Leicester City ushindi wa 1-0 na kuishika Arsenal kwa Pointi kileleni wote wakiwa na Pointi 43 kila mmoja huku Arsenal wakiwa juu kwa ubora wa Magoli.
Man City, licha ya kutoka 0-0 na Everton, wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara hao.
Mabingwa Watetezi Chelsea, wakicheza kwao Stamford Bridge, walitoka Sare 2-2 na West Bromwich Albion.
Bao za Chelsea zilifungwa na Cesar Azpilicueta, Dakika ya 20, na Gareth McAuley, Dakik a ya 73, baada kujifunga mwenyewe.
Bao za WBA zilifungwa na Gardner, Dakika ya 33, na James McClean, Dakika ya 86.

No comments:

Post a Comment