Wednesday, 6 January 2016

man city wafungwa na Everton 2- 1

Image result for CAPITAL ONE IMAGE
 
Everton wameanza vyema Nusu Fainali ya C1C, Capital One Cup, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England, kwa kuifunga Man City 2-1 Uwanjani Goodison Park.
Timu hizi zitarudiana huko Etihad hapo Januari na Mshindi kucheza Fainali na Mshindi kati ya Stoke City na Liverpool ambazo Juzi zilicheza na Liverpool kushinda 1-0.
Liverpool na Stoke zitarudiana hapo Januari 26.
Hapo Jana, Everton walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 46 la Funer Mori na City kusawazisha kwenye Dakika ya 76 kwa Bao la Jesus Navas.
Lakini Everton walinyakua ushindi kwa Bao la Dakika ya 78 la Romelu Lukaku na hilo ni Bao lake la 19 kwa Msimu huu.
 
VIKOSI;
 
Everton: Joel, Coleman, Stones, Funes Mori, Baines, Besic, Barry, Deulofeu, Barkley, Cleverley, Lukaku.
Akiba: Jagielka, Kone, Mirallas, Lennon, Osman, Howard, Galloway.
Manchester City: Caballero, Sagna, Otamendi, Mangala, Clichy, Fernandinho, Delph, Silva, Toure, De Bruyne, Aguero.
Akiba: Hart, Fernando, Sterling, Kolarov, Jesus Navas, Demichelis, Iheanacho.
REFA: Robert Madley 
 huko Etihad hapo Januari 27.
Fainali ya C1C itachezwa hapo Februari 28.

Nusu Fainali-Kanuni Muhimu:
-Kwenye Mechi za Nusu Fainali, ikiwa Jumla ya Magoli kwa Mechi 2 ni sawa baada ya Dakika 90 za Mechi ya Marudiano, Nyongeza ya Dakika 30 itachezwa.
-Ikiwa Gemu ni Sare baada ya hiyo Nyongeza ya Dakika 30, Mshindi atapatikana kwa kuhesabu Goli la Ugenini kuwa mara mbili.
-Ikiwa Gemu bado itakuwa sawa hata baada ya kuhesabu Goli za Ugenini ni mara mbili, basi Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5 kama Sheria za Soka zinavyotamka.

C1C: NUSU FAINALI:
Marudiano
**Mechi zote Saa 5 Usiku, Saa za Bongo
Januari 26
-Liverpool v Stoke City [Anfield]
Januari 27
-Man City v Everton [Etihad]
 
 

No comments:

Post a Comment