Wednesday, 6 January 2016

KOMBE LA MAPINDUZI JKU YAONGEZA UGUMU KUNDI LA SIMBA, YAITANDIKA JAMHURI 3-0

Image result for TIMU YA JKU ZANZIBAR
Mabao ya JKU jioni ya leo yamefungwa na Emmanuel Martin dakika ya tatu akimalizia krosi ya Khamis Said, Nassor Juma dakika 35 akimalizia krosi ya Ponsiana Maliki na Mohammed Abdallah dakika ya 72 akimalizia pasi ya Emmanuel Martin.
Kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili cha mchezo huo, wachezaji wa timu zote mbili na mashabiki kusimama na kuomboleza kifo cha refa mstaafu Juma Ali David aliyekuwa na beji ya FIFA  aliyefariki dunia jana mchana visiwani hapa.
Mchezo wa pili wa Kundi A unafuatia usiku kuanzia Saa 2:15 kati ya vinara wa kundi hilo, URA ya Uganda dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ya Dar es Salaam.JKU imefufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri katika mchezo wa Kundi jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Ushindi huo unaifanya JKU iokote pointi tatu za kwanza, baada ya awali kufungwa 3-1 na URA katika mchezo wa kwanza na itcheza na Simba SC mechi ya mwisho ya kukata na shoka kugombea tiketi ya Nusu Fainali.

No comments:

Post a Comment