Daktari akimpiga ngumi mgonjwa huyo.
Moscow, Urusi
Kanda
ya video ya CCTV imesambaa mitandaoni ikimuonesha daktari mmoja
aliyefahamika kwa jina la Ilya Zelendinov nchini Urusi alimpiga ngumi
mgonjwa Yevgeny Bakhtin (56) na kumuua papo hapo.
Kisa hicho kilitokea katika Mji wa Belgorod umbali wa kilomita 670 Kusini mwa Mji Mkuu wa Moscow nchini Urusi mnamo Disemba 29.Kisa kilianza kwa mgonjwa huyo kumpiga teke muuguzi mmoja kabla ya daktari huyo kumfata na kumpiga ngumi ya kichwa.
Hali ya taharuki
Vyombo
vya habari vya Urusi vimeeleza kuwa, baada tu ya kupigwa ngumi mgonjwa
huyo alizirai kabla ya kuaga dunia muda mfupi baadaye akiwa hospitalini
hapo.
Wachunguzi
wanadhani kwamba hakumuua kwa makusudi lakini wameanzisha kesi ya
uhalifu dhidi ya daktari huyo na endapo akipatikana na hatia atapelekwa
jela kosa la jinai.
Mgonjwa baada ya kuzirai.
No comments:
Post a Comment