JESHI la polisi
mkoa wa Iringa linamshikilia James Benitho (26) mkazi wa
kijiji cha Iyegela wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
kwa tuhuma za kumuua mke wake Lucy Muhusi mwenye umri
wa miaka 40 kwa kumnyonga na kumchoma na kitu chenye ncha kali
katika paja lake kisha kumtupa katika shimo la choo kwa
kile kilichoelezwa kuwa nai wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa polisi
wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema kuwa
mwanaume Benitho alifikia uamuzi huo baada ya kubaini
kusalitiwa ndoa yake kwa mwanamke huyo kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mwanaume mwingine.
Wakati huo huo mtoto
Heren Mhenzi (5) mkazi wa Isele kata ya llula barabara
ya Ilula Image wilaya ya Kilolo amepoteza maisha yake baada
ya kugongwa na pikipiki yenye namba za usajili MC156
ASR iliyokuwa ikiendeshwa na Goshen Lutambi (25) mkazi wa Mtuwa kumgonga
mtoto huyo na kusababisha kifo chake papo hapo na chanzo cha
ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva kutochukua tahadhali za
barabarani .
No comments:
Post a Comment