Takriban mateka 30
wameokolewa baada ya wapiganaji kushambulia hoteli moja katika mji mkuu
wa Ouagadougou nchini Burkina Faso na kusababisha mauaji ya takriban
watu 20.
Watu kadhaa waliofunika nyuso zao walivamia hoteli hiyo
ya Splendid,na kuwateka watu kadhaa baada ya bomu kulipuka nje ya hoteli
hiyo,kulingana na walioshuhudia.Waziri wa mawasiliano Remis Danjinou alituma ujumbe katika mtandao wa tweeter akisema takriban wtu 30 wameachiliwa huru na kwamba oparesheni ya kijeshi kukabiliana na wapiganaji hao imeanza.
Tayari takriban watu 30 wamepelekwa hosptalini wakiendelea kupata matibabu aliongezea.
Haijajulikana iwapo kuna mateka ambao bado wamesalia katika hoteli hiyo ,lakini mashahidi wameripoti milio mikali ya risasi katika ghorofa za juu mapema asubuhi.
Amesema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao haijulikani.
Afisa mkuu wa Hospitali Robert Sangare aliwanukuu baadhi ya manusura wakisema takriban watu 20 walifariki katika shambulio la kwanza,kabla ya vikosi vya usalama kuanza makabiliano na wapiganaji hao.
Kundi moja linalofuatilia mitandao ya wapiganaji wa Jihad limesema kuwa wapiganaji wa al-Qaeda katika eneo la Maghreb wamekiri kutekeleza shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment