kocha msaidizi wa zamani wa Simba, Suleiman
Matola, amesema Simba imechelewa kumtimua Kocha Dylan Kerr kwani alianza
muda mrefu kuiharibu timu
Hivi
karibuni Matola aliamua kuondoka mwenyewe Simba na kujiunga na Geita
Gold Sports ya Ligi Daraja la Kwanza kwa kile kilichoelezwa kuwa ni
kutoelewana kwake na Kerr ambaye ni raia wa Uingereza.
Simba
mapema wiki hii ilitangaza rasmi kuvunja mkataba na Kerr kwa
kilichoelezwa kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi hicho katika mechi
zake za michuano mbalimbali.
Matola
alisema: “Kerr ni kocha mzuri ila nilishawaambia viongozi mapema kuwa
hafai ndani ya timu kutokana na yeye kutaka kufuata kile anachokiamini
bila ya kushirikiana na wenzake hata kama anakosea.
“Simba
imechelewa kumtimua kwani ameiweka timu mahali pabaya na kama
angeondoka mapema usikute klabu ingekuwa pazuri sasa,” alisema Matola.
No comments:
Post a Comment