Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny.Mchezaji huyo anaweza kuwachezea dhidi ya Stoke Jumapili.
Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu Gunners £5m na anahitimu kuwachezea katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Akizungumza baada ya Arsenal kutoka sare ya 3-3 na Liverpool uwanjani Anfield, Wenger alisema: "Amejiunga nasi na tutamchunguza kuona iwapo anatosha kucheza Jumapili.”
Elneny alichezea Basel mechi ambayo walilaza Chelsea msimu wa 2013-14.
No comments:
Post a Comment