Uongozi wa Yanga, umetangaza kuvunja mkataba wake na kiungo wake Haruna Niyonzima.
Yanga imechukua uamuzi huo ikiwa ni miezi isiyozidi mitano tokea isani mkataba mpya wa miaka miwili na Niyonzima.
Msemaji
wa Yanga, Jerry Muro amesema Niyonzima atalazimika kulipa kiasi cha
dola 71,175 (zaidi ya Sh milioni 149) kutokana na kukiuka mkataba
uliosababisha kuvunjika kwa mkataba huo.
Mzozo
wa Yanga na Niyonzima ulianza baada ya kiungo huyo kuchelewa kurejea
kazini alipokwenda kuitumikia timu yake katika michuano ya Chalenji
nchini Ethiopia.
Uongozi wa Yanga ulimsimamisha kwa madai amekuwa na tabia hiyo ya kuchelewa kila mara na kumtaka atoe maelezo.
“Lakini
hata hayo maelezo hakuwasilisha kama ambavyo alitakiwa kufanya. Mwisho
hiki ndicho uongozi wa Yanga umeamua kuchukua,” alisema.
No comments:
Post a Comment