Hayo
yamesemwa hii leo katika ofisi za CHADEMA wilaya ya Iringa na na mwenyekiti wa
chama cha demokrasia na maendeleo wilaya ya iringa Frenk Nyarusi ambaye pia ni
diwani wa kata ya mivinjeni na kuongeza kuwa madiwani pamoja na viongozi wa
serikali za mitaa jukumu lao kubwa ni kuwatumikia wananchi hata bila kuhitaji
fedha kutoka kwao.
Aidha
nyarusi amebainisha kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao siyo waadilifu wamekuwa
wakijihusisha na kuomba fedha wanapotoa huduma kwa wananchi pia amesema kuwa
hawatasita kuchukua hatua kwa wale viongozi ambao watabainika na tuhuma hizo.
Hata hivyo
nyarusi amewataka madiwani kuzikumbuka ahadi walizo ahidi na kuzitekereka kwani
kutofanya hivyo watakuwa wanajiwekea mazingira magumu wao wenyewe kwenye
chaguzi zijazo.
No comments:
Post a Comment