Monday, 28 December 2015

Mchezaji auawa kwa risasi El Salvador

Image for the news result
Alfredo Pacheco

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya El Salvador Alfredo Pacheco ameuawa kwa kupigwa risasi, maafisa wanasema.Mwanamume mwenye bunduki anadaiwa kumpiga Pacheco, 33, risasi kadha katika kituo cha mafuta katika mji wa Santa Ana, kilomita 76 magharibi mwa mji mkuu wa San Salvador.
Polisi wanasema watu wengine wawili walijeruhiwa kwenye shambulio hilo, ambalo polisi bado wanachunguza dhamira yake.
Mlinzi huyo, aliyechezea El Salvador mechi nyingi zaidi za kimataifa, alipigwa marufuku maisha baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mechi 2013.
Pacheco na wachezaji wengine 13 walipatikana na hatia ya pokea hongo timu hiyo ishindwe mechi kadha kati ya 2010-13.
El Salvador, taifa ndogo lililoko Amerika ya Kati, ni moja ya mataifa yenye viwango vya juu zaidi vya mauaji.
Mapema mwezi huu, mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta, 26, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa likizoni katika mji wake wa kuzaliwa

No comments:

Post a Comment