Wednesday, 23 December 2015

Serikali ijizatiti kukomesha migogoro wakulima, wafugaji’

MBUNGE wa Viti Maalumu, Gimbi Masaba (Chadema) ameiomba serikali kujizatiti kukomesha migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikigharimu maisha ya watu na mifugo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Bariadi, alisema migogoro hiyo imekuwa na madhara makubwa kutokana na kusababisha vifo na ulemavu . Alisema serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wanapaswa kuweka mikakati ya pamoja na kudhibiti migogoro hiyo kwa kutenga maeneo ya malisho hasa kwa wafugaji waishio pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Alisema suala hilo lilipofikia si la kufumbiwa macho, hivyo mawaziri husika wanapaswa kuwajibika ipasavyo kuhakikisha wanatatua haraka matatizo yanayowakabili wananchi mkoani Simiyu.
“Hatupo tayari kuendelea kuona migogoro ya namna hii ikiendelea kuathiri maisha ya watu wakati serikali yao ipo, ni lazima sasa mawaziri husika wafanye kazi ya ziada kuondoa hili tatizo la migogoro ya mara kwa mara ya wakulima na wafugaji,”alisema.
Aidha alionya baadhi ya viongozi wa Serikali kugandamiza upande mmoja wa jamii, badala yake, waangalie uwezekano wa kuwagawia wananchi maeneo ya hifadhi za akiba na wachukue hatua za kisheria kwa viongozi na matajiri wanaopora mashamba ya wananchi masikini na kujimilikisha

No comments:

Post a Comment