Atletico Madrid wameikosa nafasi ya kuongoza La Liga baada ya Jana Usiku kufungwa 1-0 kwa Bao la Dakika ya 88 la Mbrazil Charles.
Hapo Jana, Atletico walilazimika kucheza karibu Kipindi cha Pili chote Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Gabi Fernandez kulambwa Kadi za Njano 2 ndani ya Dakika 5 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Kipigo hiki kimefuta wimbi la kutofungwa la Mechi 15 kwa Atletico na sasa wamebakia wakiwa na Pointi 35 sawa na Barcelona, ambao wamecheza Mechi 1 pungufu, lakini Barca wako juu kwa ubora wa Magoli.
Timu ya 3 ni Real Madrid, ambao mapema Jana waliinyuka Rayo Vallecano 10-2, wenye Pointi 33
La Liga sasa inaenda Mapumziko ya Siku 10 kwa ajili ya Krismasi na Mwaka mpya.
Wikiendi hii, Barca hawakucheza La Liga kwa sababu walikuwa Japan kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
No comments:
Post a Comment