SANTIAGO BERNABEU huko Madrid Leo iligeuka chereko baada ya Wenyeji Real Madrid kuitwanga Rayo Vallecano Bao 10-2 katika Mechi ya La Liga ambayo Wageni hao, walioongoza 2-1, walicheza Mtu 10 na ndipo Mvua ya Magoli kuwashukia.
Real walitangulia kufunga Bao kupitia Danilo na Rayo Vallecano kujibu kwa Bao 2 na kuongoza 2-1 lakini waliathirika mno kwa Kadi Nyekundu kwa Wachezaji wao Roberto Roman Triguero, alietolewa Dakika ya 14 na kufuatia Jose Raul Baena, Dakika ya 28.
Hadi Mapumziko Real walikwenda mbele kwa Bao 4-2.
MAGOLI:
REAL MADRID
-Danilo 3'
-G. Bale 25', 41', 61', 70'
-Cristiano Ronaldo 30', 53'
-K. Benzema 48', 79', 90’
RAYO VALLECANO
-Antonio Amaya 10'
-Jozabed 12’
Kipindi cha Pili Real waliongeza Bao 6 na hatimae kushinda Bao 10-2.
Ushindi huu umewabakisha Real Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Barcelona na Atletico Madrid ambao Leo wanaweza kuchukua uongozi ikiwa Malaga kwa vile Barca hawana Mechi kwa sababu walikuwa Japan kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
No comments:
Post a Comment