Monday, 21 December 2015
SERIE A: LAZIO WAWAPIGA VINARA INTER SAN SIRO, HIGUAIN AIBEBA NAPOLI!
Mchezaji wa Kimataifa wa Italy Antonio Candreva alipiga Bao 2 na kuipa ushindi wa 2-1 Lazio walipocheza Nyumbani kwa Vinara wa Serie A Inter Milan Uwanjani San Siro na kuwapa pigo la uongozi wao kubaki
Pointi 1 tu.
Baada ya mapema Jana Timu zinazoifuata, Fiorentina na Napoli, kushinda Mechi zao Inter Milan walitinga kwao San Siro wakitegenea ubwete ili kurejesha pengo lao la Pointi 4 kileleni dhidi ya Lazio ambayo ilikuwa haijashinda katika Mechi zao 7.
Lakini Candreva akaipa Lazio Bao la kuongoza na Mauro Icardi kuisawazishia Inter na Lazio tena kupiga Bao la ushindi kupitia Candreva katika Dakika ya 87.
Hicho ni kipigo cha 3 kwa Inter katika Mechi 17 na wanaongoza Serie A wakiwa Pointi 1 mbele ya Fiorentina na Napoli, Pointi 3 mbele ya Mabingwa Watetezi Juventus na 4 mbele ya AS Roma ambao wako Nafasi ya 5.
Hapo Jana, Napoli ikicheza Ugenini, iliichapa Atalanta Bao 3-1 na kujichimbia Nafasi ya 3.
Bao za Napoli zilifungwa na Marek Hamsik, kwa Penati, na Bao 2 za Gonzalo Higuain huku Bao la Atalanta likifungwa na Alejandro Gomez.
Serie A sasa inaenda Mapumziko ya Krismasi na Mwaka mpya na itarejea Januari 6
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment