José
Mourinho amesema hatachukua Likizo ili kupumzika baada ya kutimuliwa
Chelsea hivi Juzi bali atabaki Jijini London na kutua Viwanjani kusaidia
Marafiki zake.
Mawakala wa Mourinho wamesema hayo kupitia Taarifa maalum ambayo pia iliwashukuru Mashabiki wa Chelsea kwa sapoti yao.
Taarifa
hiyo ilikiri kuwa mara zote alikuwa ni Mourinho alieamua kuaachana na
Klabu lakini safari hii, kwa mara ya kwanza, ni Chelsea ndio ilimtema
Juzi Alhamisi.
Mourinho pia amesema anasikia fahari kubwa kwa kuiwezesha Chelsea kutwaa Makombe 8 katika vipindi vyake Viwili na Klabu hiyo.
Pia alisistiza kuwa hatapumzika kwa vile hasikii uchovu na hivyo anasubiri kwa hamu nini kitajiri kwake hivi karibuni.
Kwa
sababu anaipenda Soka, Mourinho atatua Viwanjani ili kufanya kazi na
kuwasapoti Marafiki zake lakini hatahudhuria Mechi kubwa ili kutoanzisha
uvumi wowote kuhusu yeye.
Mourinho
amesema atabaki Jijini London lakini ameomba faragha yake na ya Familia
yake iheshimiwa huku akisisitiza kuwa hataongea lolote kuhusu hali yake
ya sasa na kuwataka Wanahabari waheshimu hilo.
No comments:
Post a Comment