Saturday, 19 December 2015

MARTIAL APEWA TUZO ULAYA YA ‘KIJANA WA DHAHABU’ 2015!

Image result for ANTHONY MARTIAL

STRAIKA wa Manchester United Anthony Martial ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana kwa Mwaka 2015, Golden Boy, Kijana wa Dhahabu.
Licha ya Klabu yake Man United kutoshinda katika Mechi 5, wakiwa wamefungwa Mechi 2 zilizopita, na kuwa Nafasi ya kwenye Ligi Kuu England, Nyota pekee inayong’ara kwenye Timu yao ni juhudi za Anthony Martial ambae amefunga Bao 6 katika Mechi zake 19.
Martial, mwenye Miaka 20 ambae pia huichezea Timu ya Taifa ya France, ameitwaa Tuzo hii ya Golden Boy ambayo hupewa Vijana wa chini ya Miaka 21, kwa kuwabwaga Kingsley Coman wa Bayern Munich na Mchezaji wa Arsenal Hector Bellerin na kuitwaa.
Awali Listi ya Wagombea ilikuwa na Wachezaji 40 ambami walikuwepo Wachezaji webzake wa Martial wa Man United, Luke Shaw na Adnan Januzaj.
Washindi waliopita ambao huchezea England ni Wayne Rooney (2004) na Anderson (2008) kutuka Man United huku Mchezaji wa sasa wa Man City, Raheem Sterling, akiizoa Mwaka 2014 akiwa na Liverpool.
Tuzo hii ilianzishwa na Jaridala Italy, Tuttosport, Mwaka 2003 kwa kuendesha Kura lakini sasa Wanahabari zaidi ya 30 Magazeti ya L'Equipe (France), Marca (Spain) na The Times (England) wakishiriki kwenye mchakato wa kutoa Mshindi.

No comments:

Post a Comment