Jumamosi Desemba 19
Chelsea 3 Sunderland 1
Everton 1 Leicester 3
Man United 1 Norwich 2
Southampton 0 Tottenham 2
Stoke 1 Crystal Palace 2
West Brom 1 Bournemouth 2
Leicester City wameendelea kupaa kileleni mwa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Everton 3-2 huko Goodison Park na sasa wapo Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Arsenal.
Mabao ya Mechi hii yalifungwa na Lukaku, Dakika ya 32 na Mirallas, 89, kwa upande wa Everton na zile za Leicester City kupigwa na Mahrez, Dakika ya 27 na 65, zote kwa Penati, na la 3 kupitia Okazaki, 69.
Huko Stamford Bridge, wakicheza Mechi yao ya kwanza tangu wamfukuze Jose Mourinho, Chelsea waliifunga Sunderland 3-1 wakishuhudiwa na Menejao mpya Guus Hiddinck alieketi Jukwaani na Mmiliki Roman Abramovich pamoha na Mchezaji wao wa zamani Didier Drogba.
Huku baadhi ya Mashabiki wakiwazomea Wachezaji wao wenyewe, Cesc Fabregas, Eden Hazard na Diego Costa kwa madai ya kuchangia kufukuzwa kwa Mourinho, Chelsea walishinda Mechi hii bila ugumu mkubwa.
Bao za Chelsea hii Leo zilifungwa na Branislav Ivanovic, Dakika ya 5, Pedro, 13, na Penati ya Dakika ya 50 ya Oscar huku Sunderland wakifunga Dakika ya 53 kupitia Fabio Borini 53.
Ushindi huu umewapandisha Chelsea hadi Nafasi ya 15.
Huko Old Trafford, Man United walitawala Mechi yao na Norwich City lakini wakafungwa 2-1 kwa Bao za Jerome, Dakika ya 38, Tettey, 54, wakati Bao la Man United likifungwa na Anthony Martial katika Dakika ya 66.
Tottenham, wakicheza Ugenini, waliichapa Southampton 2-0 na kupanda hadi Nafasi ya 4.
Bao za Spurs zilifungwa na Harry Kane na Dele Alli.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumapili Desemba 20
1630 Watford v Liverpool
1900 Swansea v West Ham
Jumatatu Desemba 21
2300 Arsenal v Man City
No comments:
Post a Comment