June 13 2016 uongozi wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans kupitia kwa mkuu wake wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro aliweka wazi ukweli kuhusiana na taarifa za kiungo Salum Telela kuachwa na Yanga.
“Ni
kweli mkataba wa Salum Telela na Yanga umemalizika, hivyo yupo huru
kuongea na klabu yoyote nyingine au hata Yanga, ili kuangalia kama kuna
uwezekano wa kuongeza ila maamuzi yapo mikoni mwake” >>> Jerry Muro
Leo July 25 2016 mitandao mbalimbali ya soka Tanzania ikiwemo na mitandao ya kijamii imeandika good news ya kiungo huyo kufanikiwa kupata timu mpya, Telela baada ya kuachwa na Yanga hakuwa na timu ila leo amefanikiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Ndanda FC ya Mtwara.
No comments:
Post a Comment