MICHEZO

 

CHELSEA: ANTONIO CONTE AMEANZA HIMAYA, JOHN TERRY ABAKI KEPTENI, ACHEZE AU ASICHEZE


Image result for CHELSEA: ANTONIO CONTE

MENEJA MPYA wa Chelsea ameanza himaya yake kwa kusisitiza John Terry anabaki kuwa Kepteni wa Timu hata kama hachezi.
Mwezi Mei, kukiwa na hatihati kuwa mwisho wa Terry umefika, Chelsea iliamua kumpa nyongeza ya Mwaka Mmoja baada ya Mkataba wake kwisha na hii ni mara ya 3 kupata nyongeza ya aina hiyo.

Terry, mwenye Miaka 35 na ambae ameichezea Chelsea zaidi ya Mechi 700, amekuwa akisuasua Msimu uliopita na Mwezi Januari aliwahi mwenyewe kutangaza kuwa anatarajia kuondoka mwishoni mwa Msimu.
Akiongea kwa mara ya kwanza na Wanahabari mara baada ya kutambulishwa rasmi hii Leo huko Stamford Bridge kama Meneja mpya, Antonio Conte, ambae aliteuliwa kuwa Meneja wa Chelsea Mwezi Aprili wakati bado akiwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Italy na kupewa Mkataba wa Miaka Mitatu, amesema anamthamini sana John Terry.
Conte alieleza: “Ndio, John Terry ni Kepteni wa Chelsea acheze au asicheze. Daima ni Kepteni. Ni Mchezaji mzuri, mwenye haiba nzuri, na mvuto. Napenda kuongea nae kuhusu Klabu hii kwa sababu anaijua Klabu, ana moyo kuchezea Klabu hii na kwangu ni Mchezaji muhimu. Mchezaji akistahili kucheza, kwangu, atacheza tu!”

PICHA 6: Mapumziko ya Ronaldo akiwa na familia yake Ibiza Hispania

unajua hiki ni kipindi ambacho wachezaji soka duniani kote wanamalizia mapumziko ya likizo zao za soka baada ya Ligi zao kumalizika na sasa wanajiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa 2016/2017, Cristiano Ronaldo ambaye aliiongoza Ureno kutwaa Euro 2016, ametumia muda wake na familia yake mama, mwanae na ndugu zake kwenda fukwe za Ibiza Hispania mapuzikoni.


363F7A8E00000578-3689023-image-a-157_1468453403761
Portuguese European Championship winning captain, Cristiano Ronaldo, is seen on holiday in Ibiza with his family including his mother 13 July 2016. Please byline: G Tres/Vantagenews.com UK clients should be aware children's faces may need pixelating.
Portuguese European Championship winning captain, Cristiano Ronaldo, is seen on holiday in Ibiza with his family including his mother 13 July 2016. Please byline: G Tres/Vantagenews.com UK clients should be aware children's faces may need pixelating.
363E57F400000578-3689023-image-a-13_1468441154606


363F7AA200000578-3689023-image-a-161_1468453948799


HIVI NDIVYO MEDEAMA WALIVYOWASILI JIJINI DAR











Timu ya Medeama FC kutoka Ghana imewasili leo mchana jijini Dar es saalam tayari kabisa kwa mchezo wake dhidi ya Yanga SC katika kombe la shirikisho.Mchezo huo unatarajiwa kupigwa jumamosi ya wiki hii pale uwanja wa taifa.
nimekuandalia video inayoonyesha ripoti kamaili ya yaliyojiri.

 


MOURINHO AMEMUELEZEA ZLATAN IBRAHIMOVIC KWA MANENO MATATU TU

Movic vs Mourinho

Kocha wa Manchester Jose Mourinho amemuelezea kwa maneno matatu straika wake mpya Zlatan Ibrahimovic.

Mreno huyo amefanikiwa kumnasa mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan, Barcelona, AC Milan Paris Saint-Germain kwenye dirisha hili la usajili baada ya kumaliza kazi iliyompeleka nchini Ufaransa akiwa na PSG.
Wawili hao walipata wakati murua sana walipokuwa Inter Milan, na Mourinho amekanusha vikali kwamba straika huyo ni mtu mwenye maringo na majivuno makubwa.
“Nina maneno matatu tu ya kumwelezea Zlatan, ni mshindi, mfungaji hodari na vile vile ni mcheshi,” amesema Mourinho.
“Unahitaji kumwelewa kwa uzuri. Ni mcheshi sana na kama humfahamu vizuri, halafu ukasikiliza na kusoma nukuu zake basi unaweza kudhani ni mtu mwenye majivuno makubwa sana.
“Lakini ukweli ni kwamba, Zlatan ni mtu mcheshi sana. Hivyo naweza kusema kwamba, ni mcheshi, mshindi na mfungaji. Nimekuwa na furaha sana kumpata, na ni dhahiri kwamba yeye pia ana furaha kubwa kufanya kazi na mimi.”


MASTAA 9 AMBAO MICHUANO YA EURO IMEPANDISHA NA KUSHUSHA THAMANI ZAO








Roney



Kwa namna miaka ya hivi karibuni vilabu vinavyotafuta wachezaji, ni vigumu sana mchezaji ambaye hajulikani na pengine akafanya mambo makubwa kwenye michuano fulani mikubwa kwa mfano Euro au Copa America na ghafla kununuliwa na timu kubwa.


Hata hivyo uwezo binafsi wa mchezaji husika walau unaweza kupandisha thamani yake katika soko la usajili ama kushusha kabisa thamani yake.
Wafuatao ni wachezaji ambao kupitia michuano ya Euro mwaka huu thamani yao inaweza kuwa imepeanda na baadhi yao kushuka.
Wachezaji ambao thamani yao imepanda
Moussa Sissoko
Sidhani kama kuna yeyote aliyeifuatilia kwa uzuri michuano ya Euro kama atabisha juu ya hili. Sissoko amekuwa na kiwango cha hali ya juu katika michuano hii na naamini hata timu yake ya Newcastle itashangaa, kwamba uwezo wa mchezaji wao huyu ulijificha sehemu gani kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Naamini vilabu mbalimbali vitaanza kumfuatilia ili kunasa saini yake. Amecheza mpira mkubwa sana kwenye michuano ya Euro hasa katika mechi ya fainali dhidi ya Ureno licha ya timu yake kupoteza mchezo.
Kwa namna moja ama nyingine anaamini Sissoko hatabaki Ligi daraja la Kwanza England ambapo timu yake itakuwa ikishiriki baada ya kushuka daraja msimu uliopita.
Joao Mario
Mreno huyu ama hakika amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwenye michuano ya Euro mwaka huu. Joa Mario ambaye kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Sporting Clube de Portugal (Sporting Lisbon) ya nchini Ureno.
Uwezekano mkubwa wa kupaa kwenda kwenye ligi mbalimbali kubwa kama England na Uhispania endapo vilabu mbalimbali vimemtupia jicho la tatu. Tayari kuna tetesi za klabu ya Inter Milan kuanza kumnyemelea kwa dau la euro milioni 50.
Ivan Perisic
Licha ya timu yake ya Croatia kutolewa katika hatua ya 16 bora na Ureno, lakini hakuna shaka kwamba uwezo wa Perisic ulikuwa ni wa hali ya juu kabisa. Alicheza vyema kuanzia mwanzo wa mashindano mpaka pale waliotolewa.
Ivan Perisic 
Alifunga goli muhimu la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Uhispania ambapo Croatia walishinda magoli 2-1 na kuongoza kundi. Kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Inter Milan lakini muda wowote anaweza kuondoka kuelekea kwenye vilabu vyenye hadhi zaidi.
Robbie Brady
Kabla ya Michuano ya Euro mwaka huu kuanza, Brady alitoka kupata machungu baada ya timu yake ya Norwich City kushuka daraja. Alifunga goli muhimu la ushindi dhidi ya Itlay katika hatua ya makundi na goli la penati dhidi ya Ufaransa. Amekuwa akihusishwa kwa karibu kutakiwa na klabu ya Leicester City na pengine kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi anaweza kuwa amekamilisha dili hilo. Ni mchezaji anayesifika kwa upigaji mzuri wa mipira ya adhabu pamoja na kona.
Hal Robson-Kanu
Thamani yake ilikuwa ya chini sana kabla ya Michuano ya Euro mwaka huu kutokana na kuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu yake. Lakini uwezo wake kwenye timu ya taifa ya Wales umewashtua wengi. Goli lake muhimu dhidi ya Ubelgiji ni alama tosha ya ubora wake.
Tayari klabu ya Hull City imeanza mikakati ya kunasa saini yake licha ya kupata ushindani kutoka vilabu vya Beijing Guoan na Jiangsu Sunning kutoka China ambavyo vimemuahidi ofa ya mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki.Wachezaji ambao thamani yao imeshuka Arda Turan
Kabla ya Michuano ya Euro hakuwa kwenye kiwango bora kwenye klabu yake ya Barcelona. Michuano ya Euro ndiyo imezidi kuporomosha thamani yake kabisa. Ndiyo nahodha wa Uturuki lakini alishuhudia timu yake ikipoteza mechi mbili na kuibuka kwenye mchezo wa mwisho na kushinda. Baadaye aliomba radhi kwa mashabiki wao kwa kiwangokibovu cha timu yao. Kwa sasa Arda hawezi kutakiwa na klabu yoyote kubwa duniani kutokana na namna alivyoonesha kiwango chake katika siku za hivi karibuni.
Mario Gotze
Kama una kumbukumbu nzuri, huyu ndiyo mchezaji aliyefunga goli la ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka juzi dhidi ya Argentina. Kwenye klabu yake ya Bayern alikuwa hapewi nafasi kubwa katika msimu uliomalizika, na mbaya zaidi kwenye Michuano ya Euro ndipo alizikwa kabisa. Kocha wake alipenda kumtumia Mario Gomez kutokana na kuamua kutotumia tena mfumo uliokuwa ukimpa nafasi.
Alipewa nafasi kweye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ufaransa lakini hakufanya lolote. Liverpool, Borussia Dortmund na Tottenham Hotspurs wametajwa kumnyemelea, lakini kwa kiwango hiki alichoonesha inawezekana vilabu hivyo vikasitisha mipango yao ya kumnyaka.
Wayne Rooney 
Kocha wake wa sasa kunako klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema hatamtumia katika nafasi ya kiungo badala yake atampa nafasi ya ushambuliaji.
Na hii pengine imechangiwa na kiwango alichoonesha kwene Michuano ya Euro. Amekuwa mzuri katika kupiga pasi ndefu na sio kufumania nyavu tena. Timu yake ya England ilitolewa kwa aibu na timu changa ya Iceland kwa kufungwa magoli 2-1.
Adil Rami
Alianza vyema kwa kupewa nafasi ya kucheza kwenye Michuano ya Euro akiwa na timu yake ya Ufaransa. Baadaye alipata adhabu iliyomweka nje na na nafasi yake kuchukuliwa na Samuel Umtiti. Umtiti alikaba kabisa nafasi ya Rami na kuondoa nafasi yake ya kutazamwa na vilabu vikubwa. Kwa sasa anakipiga na Sevilla na pengine ataendelea kubaki pale kutokana na kutokuwa na vilabu vyovyote kutajwa kumnyemelea.



CHELSEA: ANTONIO CONTE AMEANZA HIMAYA, JOHN TERRY ABAKI KEPTENI, ACHEZE AU ASICHEZE


Image result for CHELSEA: ANTONIO CONTE

MENEJA MPYA wa Chelsea ameanza himaya yake kwa kusisitiza John Terry anabaki kuwa Kepteni wa Timu hata kama hachezi.
Mwezi Mei, kukiwa na hatihati kuwa mwisho wa Terry umefika, Chelsea iliamua kumpa nyongeza ya Mwaka Mmoja baada ya Mkataba wake kwisha na hii ni mara ya 3 kupata nyongeza ya aina hiyo.

Terry, mwenye Miaka 35 na ambae ameichezea Chelsea zaidi ya Mechi 700, amekuwa akisuasua Msimu uliopita na Mwezi Januari aliwahi mwenyewe kutangaza kuwa anatarajia kuondoka mwishoni mwa Msimu.
Akiongea kwa mara ya kwanza na Wanahabari mara baada ya kutambulishwa rasmi hii Leo huko Stamford Bridge kama Meneja mpya, Antonio Conte, ambae aliteuliwa kuwa Meneja wa Chelsea Mwezi Aprili wakati bado akiwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Italy na kupewa Mkataba wa Miaka Mitatu, amesema anamthamini sana John Terry.
Conte alieleza: “Ndio, John Terry ni Kepteni wa Chelsea acheze au asicheze. Daima ni Kepteni. Ni Mchezaji mzuri, mwenye haiba nzuri, na mvuto. Napenda kuongea nae kuhusu Klabu hii kwa sababu anaijua Klabu, ana moyo kuchezea Klabu hii na kwangu ni Mchezaji muhimu. Mchezaji akistahili kucheza, kwangu, atacheza tu!”

SAMATTA AINGIA KWENYE HISTORIA MPYA ULAYA

Mbwana 1





Mbwana Samatta ameendelea kuandika historia barani Ulaya baada ya kufunga kwenye mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya. Usiku wa Julai 14 Genk ilikuwa inacheza dhidi ya Buducnost Podgorica mchezo wa mtoano kuwania kufuzu kwenye michuano ya Europa League katika msimu huu wa 2016/17.

Pambano hilo limemalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa bao 2-0. Genk walianza kupata goli lao la kwanza dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati uliozamishwa wavuni na Neeskens Kebano.
Mbwana Samatta akaihakikishia ushindi timu yake kwa kufunga bao la pili dakika ya 79 kipindi cha pili. Nyota huyo wa Tanzania alipumzishwa dakika ya 88 na nafasi yake ikachukuliwa na Leandro Trossard.
Samatta alianza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Peter Maes akimuweka benchi Nikos Karelis anayehusishwa sana kujiunga na klabu ya Nottingham Forest ya England. Karelis aliingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya Kebano mfungaji wa goli la kwanza 

Orodha ya FIFA: Kenya na Tanzania zapanda


Kenya imepanda hatua 43 katika orodha ya hivi punde zaidi ya shirikisho la soka duniani FIFA na kuorodheshwa katika nafasi ya 86 duniani.
Hii ni kwa mujibu wa orodha ya FIFA inayoonesha kuwa Algeria imesalia kidedea barani Afrika japo inaorodheshwa katika nafasi ya 32 duniani.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ndiyo inayoongoza katika kanda ya afrika mashariki na kati.
DR Congo imeorodheshwa katika nafasi ya 59 duniani na 9 barani Afrika.
Uganda Cranes inaorodheshwa katika nafasi ya 15 barani Afrika na nafasi ya 69 duniani nafasi mbili mbele ya vigogo ya soka barani humu Nigeria.




Kenya ambayo ndilo taifa lililoimarika zaidi inaorodheshwa katika nafasi ya 86.
Harambee stars ya Kenya iliyojifurukuta na kuilaza Congo Brazzaville iliimarika hatua 43 na kuingia chini ya mataifa bora 100 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita.
Aidha hii ndiyo nafasi ya juu zaidi kwa Kenya tangu mwaka wa 2008.
Amavubi Stars ya Rwanda imeshuka hatua 8 na kuorodheshwa katika nafasi 111 duniani.



Licha ya kupanda hatua 13, Taifa Stars ya Tanzania inaorodheshwa katika nafasi ya 123
Inafatwa kwa karibu na Burundi ambayo vilevile imepanda hatua 7 na kutimia nafasi ya 125.
Ethiopia ni ya 132,
Sudan 142
Sudan Kusini 153
Mataifa ya mwisho kabisa katika orodha hiyo ya FIFA ni mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki yaani Djibouti, Eritrea na Somalia ambazo zote zinaorodheshwa katika nafasi ya 205.
Argentina ingali inaongoza duniani ikifwatwa na Ubeljiji.
Orodha ya mataifa kumi bora barani AfrikaAlgeria (32)
Ivory Coast (35)
Ghana (36)
Senegal (41)
Misri (43)
Tunisia (45)
Cameroon (53)
Morocco (54)
DR Congo(59)
Mali (61)
Orodha ya mataifa kumi bora duniani1 Argentina
2 Ubeljiji
3 Colombia
4 Ujerumani
5 Chile
6 Ureno
7 Ufaransa
8 Spain
9 Brazil
10 Italia 



No comments:

Post a Comment