Tuesday, 23 February 2016

Luis Suarez manusula asahau pasipoti yake

Arsenal karibia ibahatike na zawadi ya kushangaza kutoka kwa mshambuliaji wa kilabu ya Barcelona Luis Suarez baada ya mchezaji huyo kuaacha pasipoti yake nyumbani kabla ya timu yake kuondoka kuelekea mjini London.Haijulikani iwapo alisahau cheti hicho cha kusafiria kwa kusahau au la,lakini ni bahati mbaya kwa mashabiki wa Arsenal, mtu mmoja kutoka kilabu hiyo alitumwa kwa nyumba ya raia huyo wa Uruguay ili kuichukua na mchezaji huyo alifanikiwa kuondoka na kikosi kizima cha Barcelona.
Mshambuliaji huyo amekuwa akifanya mazoezi tayari kwa kinyanganyiro hicho katika uwanja wa Emirates nchini Uingereza siku ya Jummanne.
Washambuliaji wa Barcelona Lionel Messi,Suarez na Neymar wamefunga mabao 91 kati yao msimu huu huku Suarez akifunga mabao 41.
Mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa Nou Camp tarehe 16 mwezi Machi.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alijaribu kumsajili Suarez kutoka kilabu ya Liverpool mwaka 2013,kabla ya mchezaji huyo kujiunga na Barcelona.
Uis Suarez alisajiliwa na Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 75 mwaka mmoja baadaye,na Wenger anasema kuwa ndiye mchezaji anayeitishia Arsena

No comments:

Post a Comment