Kikosi cha Man United kilichokuwa kimeweka kambi Beijing China kwa ajili ya mechi za maandalizi ya msimu pamoja na kucheza mechi za International Champions Cup, Man United wameondoka jioni ya July 25 baada ya kushindwa kucheza mechi yao na Man City kutokana na hali ya hewa na hali ya uwanja kuwa mbovu.
Man United wameshindwa kucheza mechi yao ya tatu ya mashindano ya ICC dhidi ya Man City baada kuahirishwa, Man United walicheza mechi yao ya kwanza na Wigan na kuifunga goli 2-0, lakini mechi ya pili dhidi ya Borussia Dortmund walifungwa goli 4-1.
Kufutia kushindwa kucheza mchezo huo kocha Jose Mourinho, msaidizi wake Rui Faria pamoja na wachezaji wa Man United walionekana wakiingia kwenye basi kinyonge na kuanza safari ya kuondoka Beijing.
No comments:
Post a Comment