Monday, 25 July 2016

MAKOCHA WATANO BORA KUWAHI KUFUNDISHA TIMU YA TAIFA ENGLAND


England Managers




Sam Allardyce ni kocha wa kumi na tatu kuifundisha timu ya taifa ya England . Ukiwaondoa Sven Goran Eriksson raia wa Sweden na Fabio Capello kutoka Italia, makocha wengine wote walikuwa na asili ya Uingereza. Lakini katika orodha hiyo ni makocha watano tu ambao unaweza kusema walipata mafanikio ya kujivunia, je unawajua ni makocha gani hao? Makala hii inakupa majina ya makocha hao na mafanikio yao

  1. Alf Ramsey (1963 – 1974)
England Manager 1
Huyu ni kocha wa kwanza kushinda kombe la dunia akiwa na England. Tangu ushindi huo wa dunia mwaka 1966, kwenye mashindano yaliyofanyika England, timu ya taifa ya England haijawai kushinda tena kombe la dunia.
England ilikuwa moto wa kuotea mbali kipindi hicho, miaka miwili baadae walifanikiwa kufika nusu fainali ya kwanza ya mashindano ya Uefa Euro 1968.
  1. Bobby Robson (1982 -1990)
England Manager 2
Chini ya Sir Bobby Robson England ilifanikiwa kushika nafasi ya nne kombe la dunia mwaka 1990 nchini Italia. England ilipoteza nusu fainali dhidi ya Ujerumani kwa penati 3- 4 baada ya sare 1-1. Kwenye mechi ya mshindi wa tatu wakapoteza tena mbele ya wenyeji Italia
Kabla ya hapo, kwenye kombe la dunia mwaka 1986, England chini ya Bobby Robson ilitolewa robo fainali dhidi ya Argentina 2-1. Kwa magoli ya Diego Maradona moja likiwa la mkono wa Mungu
  1. Terry Venables (1994 – 1996)
England Manager 3
Mwaka 1996 wakati England ikisherekea miaka 30 tangu ushindi wa kombe la dunia wa mwaka 1996, waliandaa mashindano ya Uefa Euro. Wakiwa na matumaini makubwa baada ya kufanya kwenye Euro ya mwaka 1992, kwa bahati mbaya wakakutana tena na wababe wao Ujerumani kwenye mechi ya nusu fainali na kupoteza tena kwa penati baada ya sare 1-1
  1. Sven Goran Eriksson (2001- 2006)
BADEN-BADEN, GERMANY - JUNE 28: Sven Goran Eriksson the England head coach watches training at England's World Cup base on June 28, 2006 in Baden-Baden, Germany. (Photo by Ross Kinnaird/Getty Images)
Kocha wa kwanza raia wakigeni kuifundi Uingereza. Chini ya Eriksson England licheza robo fainali tatu mfululizo za mashindano makubwa, Kombe la dunia 2002, Euro 2004 pamoja na Kombe la dunia 2006. Kwa muda ambao Eriksson aliifundisha England aliwahi kupoteza mechi tano tu za mashindano
  1. Walter Winterbottom (1946 -1962)
England Manager 4
Ni kocha wa kwanza kufundisha timu ya taifa ya England. Kwa kipindi kile hakuwa na mamlaka kamili ya kuchagua wachezaji wa timu ya taifa. Alitengeneza timu nzuri ya vijana iliyofika robo fainali kombe la dunia mwaka 1962.
Makocha wengine ambao waliwahi kupata nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza ni
  1. Revie (1974- 1976)
  2. Ron Greeword 1976 -1982)
  3. Graham Taylor (1992 -1993)
  4. Glenn Hoddie (1996-1990)
  5. Kevin Keegan (2000)
  6. Steve Mc Claren (2007)
  7. Fabio Capello (2008 -2012)
  8. Roy Hodgson (2012- 2016)

No comments:

Post a Comment