Wakati mashabiki wengi wa Manchester United wakiwa na hasira na hofu baada ya leo asubuhi kushuhudia mchezaji ambaye alikuwa akihusishwa na kujiunga na Man United kwa muda mrefu Renato Sanchez akijiunga na Bayern Munich, jambo lilopelekea uvumi wa kocha Jose Mourinho kujiunga na United kuingia shakani, jioni ya leo kocha wa zamani wa United na mjumbe wa bodi Sir Alex Ferguson leo jioni ameonekana akitoka kwenye kikao cha siri na kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pachettino.
Ferguson na Pochettino walionekana wakitoka kwenye kikao chao jioni ya leo katika mgahawa wa Mayfair.
Pochettino ni mmoja wa makocha ambao wanapewa nafasi ya kumrithi Louis van Gaal pale Old Trafford mwishoni mwa msimu huu pamoja na kwamba tayari amekubaliana kimsingi na Spurs kuendelea nao mpaka 2021.
Kocha huyo wa zamani Southampton aliukosa ubingwa wa EPL ulioenda mikononi mwa Leicester na kuiongoza kwake vizuri Spurs kumewavutia maboss wa United na namna alivyoweza kuwaongoza vijana wadogo akiwemo mchezaji bora chipukizi Dele Alli.
Hata hivyo, Jose Mourinho bado anabaki kocha anayepewa nafasi ya kumrithi Van Gaal pale Theatre of Dreams baada ya kunyimwa kazi mwaka 2013.
Kocha msaidizi wa United Ryan Giggs na kocha wa Paria Saint Germain Laurent Blanc wamekuwa wakitajwa kuweza kurithi hiyo nafasi, ingawa kuna uwezekano mkubwa sasa kwamba huenda Van Gaal ataruhusiwa kuendelea na msimu mmoja mwingine.
No comments:
Post a Comment